ebook img

Maisha ya Hadhrat Nuruddin - Ahmadiyya Muslim Community PDF

300 Pages·2012·1.05 MB·Swahili
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview Maisha ya Hadhrat Nuruddin - Ahmadiyya Muslim Community

HADHRAT MAULAWII NURUDDINra KHALIFATUL MASIHI I NA Muhammad Zafrullah Khanra Mfasiri Jamil R. Rafiq Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania HADHRAT MAULAWII NURUDDINra KHALIFATUL MASIHI I © Islam International Publications Ltd. Chapa ya Kwanza ya Kiswahili: 2008 Nakala: 2000 Kimeenezwa na: Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya, Tanzania Mnazi mmoja, Dar es Salam. Simu: +255222110473 Fax: +255222121744 Kimechapwa na: Ahmadiyya Printing Press Dar es Salam. Tanzania Simu: +255222111031 ISBN 9987 - 438 - 08 - 3 ii HADHRAT ALHAAJ MAULAWII NURUDDINRA KHALIFATUL MASIHI I iii iv YALIYOMO YALIYOMO . ... ... ... ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... v MAELEZO YA MWENEZI .. .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... vi KUHUSU MWANDISHI .. ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... vii NENO LA MBELE ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ix MANDHARI YA NYUMA ... .. . ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... 1 KATIKA UTAFUTAJI WA ELIMU ... .... ... ... ... ... ... .... 8 KUKAA BHOPAL ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 19 WASAA MZURI WA KWENDA HIJAZI ... ... ... .... 30 TABIBU MJINI BHERA ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 42 MGANGA WA MAHARAJA . . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 52 MTAFUTA NA MTAFUTWA ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... 67 KUHAMA .... ... ... ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 81 MFUASI BORA HALISI ... .. . ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... 88 MTAALAMU MTUKUFU ... .. . ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... 96 MSHAURI MWENYE BUSARA ... .... ... ... ... ... ... .... 114 KHALIFATUL MASIHI .... ... .. . ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... 133 CHEO CHA KHALIFA .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 149 UKHALIFA .... ... ... ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 171 UGONJWA .... ... ... ... ... ... .... ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 198 MAWAIDHA YA MWISHO .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 216 KUMBUKUMBU LANGU ... .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 246 MANDHARI YA MWISHO .. . ... ... ... .... ... ... ... ... ... .... 267 v MAELEZO YA MWENEZI Sir Muhammad Zafrullah Khan r.a. aliandika kitabu katika lugha ya Kiingereza kiitwacho ‘Hadhrat Maulawii Nuruddin r.a.’ juu ya maisha ya Khalifatul Masihi I, kilichochapishwa zamani. Kitabu kinaeleza kwa urefu na mapana historia ya Al-Haj Hadhrat Hakim Maulana Nuruddin r.a. Maulana Sheikh Jamil R. Rafiq, Amir na Mbashiri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Kenya, amekifasiri kitabu hicho kwa Kiswahili. Tafsiri hii inaonyesha taaluma yake ya hali ya juu na ya ajabu sana ya lugha ya Kiswahili. Tafsiri hii ya Kiswahili ilisomwa kwa makini na Sheikh Muzaffar Ahmad Durrani na Sheikh Mubarak Mahmud wabashiri wa zamani wa Tanzania, ambao wakatoa baadhi ya mashauri mema. Vile vile katika kukamilisha kazi hii Bwana Muhammad Shafiq Sehgal, Bwana Farrukh Javed na Bwana Sherifu Tanwir Mujtaba wakasaidia kwa njia mbalimbali. Tafsiri hii ni tunda la ‘Dawati la Kiswahili’. Mfasiri na wote walioshughulikia kazi hii kubwa wanastahili kuombewa. Mwenyezi Mungu Awajalie malipo bora na Akubali juhudi na huduma yao. Amin. Ch. Muhammad Ali, Wakilut Tasnif, Tahrike Jadid, Rabwah Pakistan. 20 Aprili, 2008. vi KUHUSU MWANDISHI Sir Muhammad Zafrullah Khan r.a. (1893-1985), Sahaba wa Masihi Aliyeahidiwa a.s, mtu mwenye ufahamu na uwezo wa ajabu sana wa kukumbuka, msemaji mzuri, mwandishi sana na mtaalamu wa hali ya juu wa mtaala wa kulinganisha dini mbalimbali, alizaliwa nyumbani mwa Ch. Nasrullah Khan mjini Sialkot. Aliungana na Uahmadiyya, pamoja na wazazi wake, kwa mkono wenye baraka sana wa Masihi Aliyeahidiwa a.s. mnamo mwaka 1904. Alisoma katika shule ya msingi Municipal Board School, kisha American Mission High School. Ingawaje alikuwa hana afya njema, akapata kuwa wa kwanza katika shule katika mtihani wa darasa la kumi alipokuwa mwenye umri wa miaka kumi na minne. Akapata shahada baada ya kufaulu mtihani wa chuo kikuu (katika daraja I) katika Government College Lahore mnamo 1911, na alikuwa mwanafunzi wa kwanza kutoka India aliyepata kuwa wa kwanza katika London University katika mtihani wa mwisho wa L.L.B. mnamo 1914. Alianza kufanya kazi ya uwakili mjini Sialkot katika mwaka 1915. Ijapokuwa mdogo wa umri na uzoefu, akachaguliwa kuwa mwalimu kufundisha katika Chuo cha Sheria Lahore mnamo 1919. Alianzia kazi kama mwanasiasa akateuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la kutunga Sheria la Panjab mnamo mwaka 1926. Alifanikiwa kutetea kesi ya Waislamu katika Baraza la ‘Meza ya Duara’ lililofanyika huko London mnamo 1930, 1931 na 1932. Alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Indian Muslim League mnamo mwaka 1931. Kwa miaka sita alikuwa mwanachama wa Halmashauri ya Gavana-Jenerali ya British India na alihudumia katika nyanja mbalimbali kama vile afya, uchumi, maarifa ya mambo ya kale, reli na kadhalika. Katika kipindi hicho alihudumia kama mjumbe wa India isiyogawanyika katika mabaraza mbalimbali huko ng’ambo na akapata fursa ya kutoa fikra ya Mataifa-Mawili mbele ya wakuu wa vii nchi nyingi. Ndiyo sababu siku zote yeye na wenzake akina Qaide Azam Muhammad Ali Jinnah walikuwa ni miongoni mwa watu waliotegemewa. Alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje mnamo 1947, na kwa miaka mingi aliongoza Pakistan katika Baraza kuu La Umoja wa Mataifa. Alikuwa Mwenyekiti wa kipindi cha kumi na Saba cha Baraza Kuu La Umoja wa Mataifa. Akakamilisha kazi yake yenye sifa akiwa jaji wa korti ya Mataifa mjini Hague, Uholanzi (1954-1961), kwanza akiwa Makamu wa Raisi (1958-1961) kisha Raisi kutoka 1970 hadi 1973. Miongoni mwa maandiko yake kuna Tafsiri ya Kurani Tukufu kwa Kiingereza, Riyadhus Salihina (kitabu cha Hadithi) kwa Kiingereza na Tadhkirah (mkusanyiko wa wahyi, ruya na kashfi za Masihi Aliyeahidiwa a.s.) pia kwa Kiingereza. Aidha, aliandika zaidi ya dazeni ya vitabu juu ya mambo mbalimbali kuhusu dini na siasa. viii NENO LA MBELE Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s, Masihi aliyeahidiwa na Imam Mahdi, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiya, alifariki baada ya kuugua kwa masaa machache, tarehe 26 Mei 1908, mjini Lahore. Yeye alipokea habari za ukaribu wa kufariki kwake kwa njia ya ufunuo aliofunuliwa na Mungu majuma kadha kabla. Hata hivyo, habari hizi zilipotimia za kifo chake wanajumuiya walipata pigo kubwa mioyoni mwao. Wapinzani wake wakali wakafarijika, na wale waliokuwa wabaya zaidi walifanya shangwe isiyofaa kwani walidhani kwa vyovyote hatari kubwa kabisa kwa baadhi ya itikadi na imani zao na kwa mienendo yao waliyoyazoea iliondolewa. Wakadhani kwamba Jumuiya aliyoanzisha haraka itazikwa katika historia na itasahaulika kama kiwimbi kisichofungamana juu ya uso wa imani sahihi ya Islam. Wenye busara miongoni mwa Waislamu, ingawaje hawakukubaliana na madai yake, walihisi kwamba wamefiwanashujaa mkubwa wa Islam ambaye kifo chake ni hasara kubwa isiyoweza kurekebishwa. Hata wasiokuwa Waislamu walikiri na kuusifu sana utaalamu wake, unyofu wake mkubwa na uhalisi na wema wa maisha yake. Katika wakati huo muhimu sana katika historia ya Jumuiya, ya dini, na ya binadamu, kabla hajazikwa yeye huko Qadian tarehe 27 Mei, Hadhrat Maulawii Nuruddin alitangazwa kuwa Khalifa wake wa kiroho ambaye alikuwa mfuasi wake mkuu na mwaminifu wa hali ya juu, aliyeipenda ajabu Kurani Tukufu, naye alikuwa pia tabibu maarufu sana. Wanajumuiya wote walifanya baiati kwake akiwa Khalifatul Masihi. Akiwa na cheo hicho, yeye aliwajibikiwa ix kutekeleza kazi ile aliyowajibikiwa kutekeleza Hadhrat Abu Bakr r.a., Khalifa wa kwanza wa Mtume Mtukufu s.a.w. wa Islam wakati wa hatari kubwa zaidi kwa Islam na kwa binadamu, miaka elfu moja na mia tatu hapo kabla. Mungu Mhisani akamjalia Hadhrat Maulawii Nuruddin kutekeleza kazi hiyo vizuri sana hata kwamba wakati wa kifo chake kilichotokea mnamo Machi 1914, Jumuiya iliyokwisha timiza robo karne mpaka wakati huo, ilikuwa imekwisha imarika na kukingwa isiweze kuvunjika na kusambaratika. Majaribio ya jambo hili yakaja haraka kwa sura ya tambio ya hatari kwa kawaida yenyewe ya kuwepo kwa Ukhalifa kutokana na wanajumuiya kadha mashuhuri waliodai kwamba wanajumuiya asilimia 95 wanawaunga mkono. Lakini muda si muda wakafumbuliwa macho. Sehemu kubwa zaidi ya Jumuiya ikaipinga tambio vikali na kwa imara, na Jumuiya inaendelea kusonga mbele ikipata ushindi baada ya ushindi chini ya uongozi mwema na wenye hekima na ulezi bora wa Hadhrat Khalifatul Masihi II (1914-1965) na Hadhrat Khalifatul Masihi III. Hadi sasa matawi yake yameenea duniani kote, na idadi ya wanajumuiya inayoongezeka kila siku inazidi milioni kumi. Inatambuliwa sana kuwa ni ufufuo wa Islam uliokuwa umeahidiwa na Mungu (9:33). Daraja la Hadhrat Maulawii Nuruddin, Khalifatul Masihi I r.a. limeimarika barabara katika historia ya Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya. Lakini wale wanajumuiya na wengine watafutao ukweli wasiojua Kiurdu hawajui sana kuhusu maisha na khulka zake. Hili ni jaribio la kueleza kidogo sana habari hizo. Kwa njia hii mwandishi anataka kulipa sehemu ndogo sana ya deni kubwa la kumtolea shukrani analowiwa na mtu huyu mpendwa mwenye adhama, mtukufu, maarufu na mkarimu ambaye kutoka kwake mwandishi alipata baraka nyingi na ukarimu mwingi. Mwandishi amechukua maelezo karibu yote, isipokuwa mlango x

Description:
wa Halmashauri ya Gavana-Jenerali ya British India na alihudumia ya kuwepo kwa Ukhalifa kutokana na wanajumuiya kadha mashuhuri waliodai kwamba .. Kambi la Gunnah, mara wakaonywa na mkulima mmoja kubadilisha njia yao
See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.